Main Title

source : parstoday
Jumapili

5 Desemba 2021

15:35:48
1205471

Sheikh Zakzaky aadhimisha kumbukumbu ya mauaji ya Zaria

Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky amewaongoza Waislamu wa Nigeria katika maadhimisho ya mwaka wa sita wa kumbukumbu ya mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa na jeshi la nchi hiyo katika mji wa Zaria jimboni Kaduna, dhidi ya wanachama wa harakati hiyo.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Sheikh Zakzaky ametuma risala za rambirambi na kuwazinyooshea mkono wa pole familia za mashahahidi waliouawa katika tukio hilo la kutisha, lililolaaniwa ndani na nje ya Nigeria miaka sita iliyopita.

Kadhalika mwanaharakati huyo wa Kiislamu ambaye ni mtetezi wa wanyonge sanjari na kuziomba familia za wahanga wa mauaji hayo kuwa na subira na kukubali kadari ya Allah, amezitaka kuwakumbuka daima wapendwa wao waliouawa shahidi.

Katika shambulio hilo la Disemba 12, 2015, inakadiriwa wanachama zaidi ya 1,000 wa harakati ya Kiislamu ya Nigeria, aghalabu wakiwa ni Waislamu wa madhehebu ya Shia waliuawa kwa kufyatuliwa risasi na jeshi la Nigeria. Miongoni mwa waliouawa walikuwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria.

Katika siku iliyofuata, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe Malama Zeenat walitiwa nguvuni wakati wanajeshi wa Nigeria walipovamia Hussainia ya Baqiyatullah na nyumba ya mwanazuoni huyo katika mji wa Zaria.

Hatua kandamizi na za kikatili za polisi na jeshi la Nigeria dhidi ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky zingali zinaendelea na hadi sasa idadi kubwa ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini wamewekwa kizuizini au wameuawa shahidi.

342/