Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

28 Mei 2022

12:48:01
1261683

Russia yataka maabara za kibiolojia za Marekani nchini Nigeria zichunguzwe

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetaka ufanyike uchunguzi kuhusu shughuli za maabara za kibiolojia za Marekani nchini Nigeria na maambukizi ya Ndui ya Nyani (Monkeypox) nchini humo.

Ripoti ya shirika la habari la Ahlul Bayt(as)- ABNA - Igor Krilov, mkuu wa vikosi vya Russia vinavyohusika na uzuiaji wa minunurisho na silaha za kemikali na biolojia amesema, Moscow inalitaka Shirika la Afya Duniani WHO lichunguze shughuli za maabara za Nigeria katika miji ya Abuja, Zaria na Lagos, ambazo zinagharimiwa kwa bajeti ya serikali ya Marekani.

Krilov amebainisha kuwa, kwa mujibu wa taarifa zilizopo, kuna maabara za biolojia zisizopungua nne zinazofanya kazi nchini Nigeria ambazo zinamilikiwa na Marekani; na kwa mujibu wa ripoti ya WHO Ndui ya Nyani katika eneo la Afrika Magharibi ilianzia huko Nigeria.

Kwa mujibu wa data za wizara ya ulinzi ya Russia, maabara mbili za kibiolojia zinazomilikiwa na Marekani ziko katika mji wa Abuja, na mbili zingine zinaendesha shughuli zao katika miji ya Lagos na Zaria.

Katika ripoti yake mpya, Shirika la Afya Duniani limetangaza kuwa hadi sasa limepokea ripoti za kubainika watu karibu 200 waliokumbwa na ugonjwa wa Ndui ya Nyani katika nchi zaidi ya 20 duniani.

Ndui ya Nyani husababishwa na kirusi cha familia moja ya virusi vya ndui. Dalili za awali za ugonjwa huo ni pamoja na homa, kuumwa na kichwa, uvimbe, maumivu ya mgongo, kuumwa misuli na udhaifu wa mwili kwa ujumla.../

342/