Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

1 Oktoba 2022

19:09:39
1309554

Putin: Wamagharibi wanataka kufanya "mapinduzi ya rangi" katika nchi mbalimbali

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema kuwa, nchi za Magharibi zinataka kuanzisha mapinduzi ya rangi na kumwaga mito ya damu za watu katika nchi mbalimbali.

Putin ametoa matamshi haya kupitia mawasiliano ya video na wakuu wa mashirika ya upelelezi ya Jumuiya ya Madola Huru.

Rais wa Russia amesema: "Tunajua kwamba nchi za Magharibi zinapanga mikakati ya kuchochea migogoro mipya katika eneo la Jumuiya ya Madola Huru."

Putin ameongeza kuwa: “Inatosha kuangalia kinachoendelea kati ya Russia na Ukraine, kinachoendelea kwenye mipaka ya baadhi ya nchi za Jumuiya ya Madola Huru. Hakika, haya yote ni matokeo ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti."

Putin amekumbusha kuwa: "Baadhi ya nchi za Magharibi, zimebakia katika kipindi kilichopita na zinajaribu kutekeleza sera zao za kuzua matatizo na migogoro mipya katika nyanja zote, kuanzia uhusiano wa kimataifa hadi uchumi, hata utamaduni na michezo."

Matamshi hayo ya Rais Vladimir Putin yametolewa huku Ikulu ya Kremlin ikitangaza kuwa leo rais wa nchi hiyo ametoa dikrii akitambua rasmi uhuru wa mikoa ya Zaporozhye na Kherson ya Ukraine.

Siku za hivi karibuni, kumefanyika kura za maoni katika mikoa minne ya wazungumzao Kirusi ambayo ni Donetsk, Luhansk, Kherson na Zaporizhia. Matokio ya kura hizo za maoni yanaonesha kuwa asilimia kubwa ya wakazi wa maeneo hayo wameamua kujitenga na Ukraine na kujiunga na ardhi mama ya Russia. 

342/