Main Title

source : Parstoday
Jumatano

5 Oktoba 2022

15:42:37
1310806

Nasser Kan'ani: Morocco iwajibike kwa madhara ya kuanzisha uhusiano na utawala haramu

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amemwambia Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Morocco kwamba anapaswa kuwajibishwa kutokana na ukosefu wa usalama unaotokana na kuanzisha uhusiano baina ya nchi hiyo na na utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendelea kuua watu wa Palestina na kukalia kwa mabavu kibla cha kwanza cha Waislamu.

Nasser Kan'ani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekanusha madai ya uwongo na ya mara kwa mara ya Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Morocco ambaye katika taarifa zake alidai kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaingilia masuala ya ndani ya Yemen na nchi nyingine za Kiarabu, na kuongeza: "Badala ya kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Morocco inapaswa kuwa na wasiwasi na kuwajibika kuhusiana na ukosefu wa usalama unaotishia nchi na mataifa ya eneo la Magharibi mwa Asia kutokana na kuanzisha uhusiano na utawala wa kibaguzi wa Israel.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amemshauri Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco kutumia muda wake kwa ajili ya kutatua matatizo, mateso na mashaka ya wananchi madhulumu wa Yemen; na badala ya kuutegemea utawala wa Kizayuni katika kulazimisha matakwa yake, itayarishe mazingira yanayofaa kwa watu wa Sahara Magharibi kujiamulia mambo yao kwa kwa mujibu wa  sheria na kanuni za Umoja wa Mataifa.

342/