Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

27 Oktoba 2022

17:27:23
1317820

Dunia yalaani shambulio la umwagaji damu nchini Iran

Jamii ya kimataifa imeendelea kutuma salamu za rambirambi na kutoa taarifa za kulaani shambulio la kigaidi lililopelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya watu kusini magharibi mwa Iran.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterrres amekosoa vikali shambulio hilo la jana Jumatano katika Haram Tukufu ya Shah Cheragh mjini Shiraz, katika mkoa wa Fars kusini magharibi mwa nchi.

Guterres kupitia msemaji wake Stephane Dujjaric amesema UN inalaani shambulio hilo dhidi ya eneo la kidini, na inaipa pole serikali na taifa la Iran kufuatia hujuma hiyo iliyosababisha maafa.

Naye Mohammad al-Houthi, mwanachama mwandamizi wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen sambamba na kuwapa pole wananchi wa Iran kufuatia shambulio hilo amesema: Tuna uhakika tukio hilo la kihaini litazidisha umoja wa Wairani, mkabala wa njama za maadui wa Iran.

Kwa upande wake, Nasser Kana'ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa undumakuwili wa unafiki wa nchi za Magharibi, kwa kuihadaa dunia kuwa zimeguswa na shambulio hilo la jana.

Amesema: Wale wanaojifanya kutetea haki za binadamu, ndio wanafuatilia matukio ya ghasia na umwagaji damu za wananchi wa Iran. Kwao wao, mwisho (wa jambo), unahalalisha njia (iliyotumiwa).

Wakati huohuo, Kiongozi wa Harakati ya Hikma ya Kitaifa ya Iraq, Ammar al-Hakim amelaani shambulio hilo la kigaidi, sambamba na kuwawaombea afueni ya haraka majeruhi wa ukatili huo.

342/