Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

3 Novemba 2022

21:15:29
1320071

Balozi Agyeman: Baraza la Usalama la UN halitaijadili Iran

Rais wa kiduru wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amejitenga na kampeni ya kidikteta ya vyombo vya habari vya Wamagharibi wakiongozwa na Marekani, vinavyoshinikiza kujadiliwa kadhia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwenye taasisi hiyo kubwa zaidi ya UN.

Akijibu suali la mwandishi wa shirika la habari  la IRNA la Iran, Harold Agyeman ambaye pia ni Balozi wa Ghana katika Umoja wa Mataifa amesisitiza kuwa, "Baraza la Usalama la UN halitafanya kikao cha kuijadili Iran."

Balozi Agyeman ameeleza bayana kuwa, kadhia ya makubaliano ya nyuklia ya Iran (JCPOA) inajadiliwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, lakini hali inayoshuhudiwa hivi sasa nchini Iran haitaangaziwa kwenye baraza hilo.

Mwenyekiti huyo wa wa kiduru wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amebainisha kuwa, chombo hicho kinafuatilia kadhia ya Iran katika ngazi ya kitaifa, na kinalitazama suala hilo katika fremu ya mamlaka ya kujitawala Iran.   

Kabla ya hapo, Amir Saied Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa alionya kuwa, kufanya kikao chini ya anuani ya "Maandamano yanayoendelea Iran" kutaacha nyuma kumbukumbu ya hatari. 

Wamagharibi wamekuwa wakichochea na kukoleza moto wa fujo na ghasia hapa nchini kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, kwa kisingizio cha kifo cha binti wa Kiirani, Mahsa Amini.

342/