Main Title

source : Parstoday
Jumatano

9 Novemba 2022

18:26:32
1321774

Inkstick: Silaha za Marekani zinatumika kuua raia wa Yemen

Vyombo vya habari vya Marekani vimefichua kwamba muungano wa vita unaoongozwa na Saudi Arabia unatumia silaha zilizotengenezwa Marekani kuua raia wa Yemen.

Kituo cha habari cha "Inkstick" huko Marekani kimeripoti kuwa raia wasio na hatia wa Yemen wanauawa kwa silaha za Marekani na kuongeza kuwa: Mbali na mazoezi mengine yaliyofanywa katika ardhi ya Marekani, Kikosi cha Anga cha Marekani pia linafanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi kwa kushirikiana na kwa uchache asilimia 80 ya wanaanga wa Saudia katika vita dhidi ya watu wa Yemen.

Tovuti hiyo ya habari iliyobobea katika masuala ya kigeni imeeleza kuwa, kuiuzia Saudi Arabia silaha za Marekani ni hatari ya kimaadili nchini Yemen na kuongeza kuwa: Kadiri Washington inavyotuma silaha ndivyo raia wasio na hatia wanavyozidi kuuawa na Saudi Arabia nchini Yemen, na jambo hili linaifanya Washington kuwa mhusika katika ukiukaji wa haki za binadamu.

Inkstick amesema kuwa, maoni ya umma yanataka kukomeshwa mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia, kwani uchunguzi wa maoni  uliofanywa hivi majuzi na Taasisi ya Eurasia Group ulionesha kuwa karibu asilimia 70 ya Wamarekani wanapinga kutumwa silaha huko Saudi Arabia.

Huku kikiashiria kwamba maafa ya haki za binadamu yanayofanywa na muungano wa Saudi Arabia huko Yemen ndio makubwa zaidi ya binadamu katika karne ya 21, chombo hicho cha habari cha Marekani kimeitaka serikali ya Washington kuacha mara moja kuiuzia Saudi Arabia silaha na kufanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi na nchi hiyo.

Baada ya miaka saba ya kuivamia Yemen, kuua maelfu ya watu na kuharibu miundombinu ya nchi hiyo, Saudi Arabia na washirika wake zimeshindwa kufikia malengo yao, na zimelazimika kukubali kusitishwa mapigano baada ya mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani za wanajeshi na wapiganaji wa harakati ya Ansarullah wa Yemen.

342/