Main Title

source : Parstoday
Jumatano

9 Novemba 2022

18:27:02
1321775

Ripoti: Tel Aviv inatumia "mbinu za kimafia" dhidi ya makundi ya haki za binadamu ya Palestina

Shirika la kutetea haki za binadamu la Palestina limesema katika ripoti yake kwa kamati ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa kwamba Israel inatumia vitisho na mbinu za kimafia kuyanyamazisha mashirika ya kutetea haki za binadamu.

Kundi la wanaharakati wa haki za binadamu wa Palestina limeiambia kamati ya Umoja wa Mataifa kwamba katika fremu ya unyanyasaji uliopangwa, Israel inatumia vitisho na "mbinu za kimafia" kuyanyamazisha makundi ambayo yanaamini kuwa utawala huo unakiuka haki za binadamu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, utawala wa Kizayuni wa Israel unapinga shughuli zote zinazofanyika chini ya usimamizi wa kamati ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa na unadai kuwa ni bandia.

Shawan Jabarin, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la wanaharakati wa kutetea haki za binadamu la "Al-Haq", amesema kuwa vikosi vya usalama vya Israel vimekuwa vikilinyanyasa na kutumia mbinu za kimafia dhidi ya shirika hilo katika miaka kadhaa ya hivi karibuni.

Jabarin ameongeza kuwa: Israel imetumia kila njia, ikiwa ni pamoja na rasilimali za kifedha, kampeni ya kuchafua jina la shirika hilo na vitisho na hatimaye ilifunga ofisi yake eneo la Bab Maadani mnamo Agosti 18.

Siku chache zilizopita, Gilad Menashe Erdan, balozi wa utawala wa Kizayuni wa Israel katika Umoja wa Mataifa alilishambulia Baraza la Haki za Binadamu la umoja huo pamoja na wajumbe wa kamati huru ya uchunguzi iliyotumwa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Kamati hiyo iliundwa kufuatia ripoti zinazoushutumu utawala wa Kizayuni kwa umefanya jinai za kivita dhidi ya Wapalestina.

342/