Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

12 Novemba 2022

20:18:16
1322527

Mwandishi akamatwa kwa kuuliza swali kuhusu silaha za maangamizi za Marekani

Swali kuhusu silaha za maangamizi ya umati za Marekani limekuwa sababu ya kukamatwa kwa mwandishi wa habari huko Texas.

Marekani ni moja kati ya eti waungaji mkono wakuu wa wazo la Mashariki ya Kati isiyo na silaha za maangamizi ya halaiki, lakini kivitendo, Washington sio tu haijachukua hatua yoyote katika uwanja huu, lbali pia imechukua hatua ya kuimarisha harakati zisizo za kawaida za kijeshi katika kanda ya Asia Magharibi.

Ripoti zinasema, mwandishi wa habari "Tyler Hansen" aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: Siku ya Alhamisi, katika mkutano na waandishi wa habari huko Texas, alimuuliza maswali John Bolton, msaidizi wa zamani wa Shirika la Usalama wa Taifa la Marekani, kuhusu silaha za maangamizi za nchi hiyo huko Iraq na Afghanistan, na pia kuhusu kukamatwa Julian Assange, mwanzilishi wa WikiLeaks, na kuuliza maswali hayo kulifanya afukuzwe kwenye mkutano na waandishi wa habari na kisha kukamatwa.

Baadhi ya vyanzo vya habari vimeandika kuwa katika mkutano huo, John Bolton alikuwa akijaribu kuficha shughuli za Marekani na matumizi ya silaha za maangamizi nchini Iraq na Afghanistan, na ndipo alipohojiwa na kuulizwa maswali na mwandishi wa habari na kutuhumiwa kudanganya kuhusu habari vita vya Marekani katika nchi nyingine.

John Bolton

Mwandishi habari Hansen alisema kwa sauti kubwa kwenye mkutano huo kwamba: "Kimsingi Marekani ilifanya mauaji ya halaiki ya watu wa Iraq na sasa unafunika na kuficha uhalifu wake wa kivita nchini Afghanistan."

Mwandishi huyo wa habari aliendelea kuhoji kwamba: "Kwa nini mnasherehekea kukamatwa kwa Julian Assange?" Je, inakubalika kwako kusherehekea uhalifu wa kivita?

Baada ya maswali hayo mwandishi huyo wa habari alifukuzwa kwenye mkutanoni na kukamatwa na vyombo vya usalama vya Marekani.

342/