Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

12 Novemba 2022

20:19:21
1322529

Ujerumani yashinikiza kufungwa Kituo cha Kiislamu cha Hamburg

Baadhi ya vyama vya siasa katika serikali ya muungano nchini Ujerumani vimelikabidhi Bunge la Federali la nchi hiyo rasimu ya mpango wa kufungwa Kituo cha Kiislamu cha Hamburg.

Vyama hivyo vimedai katika rasimu hiyo kuwa, kituo hicho kinatumika kama taasisi ya kueneza fikra na misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Aidha vyama hivyo vya kisiasa vinavyounda serikali mahuluti nchini Ujerumani vinadai kuwa, mashinikizo ya kutaka kufungwa Kituo cha Kiislamu cha Hamburg ni sehemu ya kuunga mkono maandamano ya fujo nchini Iran.

Kutokana na uwepo wa lobi za utawala wa Kizayuni wa Israel na kushamiri harakati za kundi la kigaidi la MKO nchini Ujerumani, vyombo vya habari vya nchi hiyo ya Ulaya vimekuwa vikieneza propaganda dhidi ya kituo hicho cha kidini na kitamaduni mjini Humburg.

Haya yanajiri mwezi mmoja baada ya utafiti mpya uliofanywa na Baraza la Wataalamu la Utangamano na Uhamiaji la Ujerumani (SVR) kuonyesha kuwa, mitazamo hasi na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu vimeongezeka kwa kiwango cha kutia wasiwasi nchini humo.

Kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo yaliyotolewa mapema mwezi uliopita wa Oktoba, asilmia 48 ya Wajerumani wanahisi kuwa Uislamu 'hauendani' na 'thamani' za jamii ya Ujerumani.

Aidha asilimia 29 ya Wajerumani walioshirikishwa kwenye utafiti huo wanasisitiza kuwa, dini ya Kiislamu inapaswa kupigwa marufuku nchini humo. Utafiti huo ulibainisha kuwa, mitazamo hiyo ya chuki za kidini inawalenga Waislamu wa matabaka yote, wawe wahajiri au wazawa wa nchi hiyo ya Ulaya.

Hii ni katyika hali ambayo, Ujerumani yenye jamii ya watu milioni 84, ndilo taifa la pili lenye idadi kubwa zaidi ya Waislamu Ulaya Magharibi baada ya Ufaransa. Nchi hiyo ina Waislamu karibu milioni 5, na idadi hiyo inaongezeka kwa kasi kubwa. 

342/