Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

12 Novemba 2022

20:21:18
1322532

Qatar yasisitiza tena kupinga kuanzisha uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel

Serikali ya Qatar kwa mara nyingine tena imesisitiza msimamo wake wa kupinga kuanzisha uhusiano wa kawaida wa aina yoyote ile na utawala wa Kizayuni wa Israel unaofanya mauaji kila leo huko Palestina.

Duru za habari za Kizayuni zimetangaza kuwa, serikali ya Qatar haitaki kabisa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israela na kwamba, Dohha inaendelea kusisitiza kwamba, kwamba, suala hilo linafungamana na kupendekezwa mpango wa kuipatia ufumbuzi kadhia ya Palestina.

Kiongozi mmoja wa Qatar amesisitiza kuwa, msimamo wan chi yake kuhusiana na kuuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel haujabadilika.

Qatar ni miongoni mwa mataifa machachev ya Kiarbu yenye msimamo mzuri kuhusiana na suuala la Palestina.

Hivi karibuni serikali ya Qatar ilikataa ombi la utawala haramu wa Israel la kuanzishwa ubalozi mdogo wa muda wa Israel mjini Doha katika kipindi cha kufanyika fainali za soka za Kombe la Dunia. 

Viongozi wa Doha walikataa ombi hilo ambalo kwa mujibu wa viongozi wa Tel Aviv lililenga kufungua ubalozi wake mdogo wa muda mjini Doha kwa ajili ya kushughulikia masuala mbalimbali ya mashabiki wa Israel ambao wataelekea nchini humo kwa ajili ya kushuhudia mashindano hayo.

Ikumbukwe kuuwa, mwezi Disemba mwaka 2020 Morocco ilijiunga na Imarati, Bahrain na Sudan katika kuanzisha uhusiano rasmi na utawala haramu wa Israel chini ya upatanishi wa Marekani. Mapatano hayo yanaendelea kulaaniwa ndani ya nchi hizo za Kiarabu na ulimwengu wa Kiislamu kwa ujumla kwani ni usaliti kwa malengo matukufu ya ukombozi wa Palestina.


342/