Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

12 Novemba 2022

20:23:16
1322536

Kuwait: Israel inapaswa kuweka vituo vyake vya nyuklia chini ya usimamizi wa IAEA

Kwa mara nyingine tena Kuwait imeutaka utawala haramu wa Israel ujiunge na Mkataba wa Kuzuia Usambazaji wa Silaha za Nyuklia (NPT) na kuweka vituo vyake vyote vya nyuklia chini ya mfumo wa usimamizi wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Katika taarifa iliyowasilishwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, serikali ya Kuwait imeeleza dhamira yake ya kuanzisha eneo lisilo na silaha za nyuklia na silaha nyingine za maangamizi katika Mashariki ya Kati kulingana na azimio la mkutano wa mapitio ya Mkataba wa Kuzuia Silaha za Nyuklia na matokeo ya makongamano ya 2000 na 2010.

Ahmed Salmin, mjumbe wa timu ya Kuwait katika Umoja wa Mataifa, amewasilisha taarifa ya nchi yake kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati wa mapitio ya "Ripoti ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki", ambapo amesisitiza umuhimu wa Israel kijiunga na Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia. Amesisitiza kuwa taasisi zote za nyuklia za utawala huo zinapaswa kuwa chini ya usimamizi kamili wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki.

Nchi 152 za ​​dunia tayari zimeutaka utawala wa Kizayuni wa Israel ujiunge na Mkataba wa Kuzuia Uenezaji wa Silaha za Nyuklia (NPT).

Mkataba wa NPT umetiwa saini na nchi wanachama 186 za dunia.

342/