Main Title

source : Parstoday
Jumapili

13 Novemba 2022

15:52:08
1322828

Kukabidhiwa watoto wa kike wa Kiislamu kwa mashoga nchini Uswidi kwazua wimbi la malalamiko

Mkanda wa video uliorushwa hewani kupitia mitandao ya kijamii kuhusu mashoga wawili waliopewa haki ya kulea mtoto wa kike wa Kiislamu umeibua hasira za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii katika nchi za Kiislamu.

Wakimbizi katika nchi za Ulaya wanakabiliwa na mateso na changamoto mpya. Katika mkondo huo inaripotiwa kuwa, iwapo Idara ya Masuala ya Kijamii ya Uswidi itaamua kwamba wazazi wahajiri wa mtoto hawana uwezo wa kulea au kukaa na mtoto huyo, itamchukua kutoka kwa wazazi wake na kuwapa familia nyingine. Wakati mwingine watoto hao huwekwa chini ya usimamizi wa mashoga na mabaradhuli. 

Maryam ni jina la msichana wa Kiislamu mwenye umri wa miaka mitano ambaye alikabiliwa na mkasa kama huu bila kukusudia wala kujua.

Gazeti la "Aftonbladet" la Uswidi limeripoti kuwa, mashoga wawili wenye majina ya "John" na "Johan" wamepewa haki ya kumlea msichana huyo mdogo wa Kiislamu kutoka Idara ya Masuala ya Kijamii ya Uswidi. Idara hiyo imewanyang'anya wazazi wawili wa msichana huyu Mwislamu haki ya kulea mtoto wao na kutangaza kuwa mashoga hao ndio wanaostahili kumlea Maryam.

Inafaa kusema hapa kwamba, Maryam alichukuliwa kwa nguvu kutoka kwa familia yake alipokuwa na umri wa miezi 10 tu, na kuwekwa chini ya ulezi wa mashoga hao wawili.

Ripoti zinaonyesha kuwa, Idara ya Masuala ya Kijamii ya Uswidi imekuwa ikitoa haki ya ulezi wa watoto wa wahajiri Waislamu kwa mashoga na mabaradhuli wa nchi hiyo.

Wakimbizi wanaoelekea Ulaya

Kuchapishwa kwa habari hii kwenye vyombo vya habari kumeibua hisia na upinzani mkubwa katika nchi za Kiislamu. Baadhi ya watumiaji wameandika kwamba Sweden, kinyume na taswira yake, ni nchi katili, ya kibaguzi ambayo haikufaidika na demokrasia na sera za kulinda haki za watoto.

Watumiaji wengine wameandika kwamba Sweden na nchi zingine za Magharibi zinawafinyia binadamu mambo ambayo hayafanyiki hata katika vita.

Kitendo kama hicho kilichofanywa na Idara ya Masuala ya Kijamii ya Uswidi kimefanyika pia nchini Ujerumani. Familia moja ya wahajiri wa Kituruki imeripoti kuwa imenyang'anywa mtoto mwenye umri wa miezi kumi na kukabidhiwa kwa mashoga wawili katika mji wa Aachen. 

342/