Main Title

source : Parstoday
Jumanne

15 Novemba 2022

16:41:05
1323355

Marekani yaitaka Ukraine ifanye mazungumzo ya amani na Russia

Maafisa wa ngazi za juu wa Marekani wameanzisha kampeni ya kuishawishi Ukraine itafakari juu ya suala la kufanya mazungumzo ya amani na Russia, wakihofia kuwa msimu wa baridi kali yumkini ukaikwamisha serikali ya Kiev baada ya eti kupata ushindi wa kulidhibiti tena eneo la Kherson.

Gazeti la The Wall Street Journal la Marekani limeripoti kuwa, licha ya ahadi za Marekani na waitifaki wake za kuipa Ukraine silaha na misaada mingine ya kijeshi, lakini maafisa waandamizi mjini Washington hivi sasa wameanza kutafakari kuhusu gharama za vita vya Ukraine.

Miongoni mwa maafisa wa ngazi za juu wa Marekani walionukuliwa na gazeti hilo ni Mkuu wa Majeshi ya US, Jenerali Mark Milley, ambaye hivi karibuni alisema, iwapo mafanikio yaliyokusudiwa hayapatikani kupitia njia za kijeshi, kuna fursa ya kutumia njia za mazungumzo.

Inaarifiwa kuwa, Marekani imetumia zaidi ya dola bilioni 19 katika msaada wa kijeshi kwa Ukraine hadi sasa mwaka huu, ikiipiku kwa mbali misaada ya nchi za Ulaya kwa Kiev. 

Haya yanajiri siku chache baada ya Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Russia, Dmitry Medvedev kusema, Moscow ina silaha za ziada katika maghala yake kwa ajili ya matumizi vitani Ukraine.

Kremlin yasisitiza kuwa Kherson itasalia kuwa milki ya Russia

Russia ilianzisha "operesheni maalum ya kijeshi" nchini Ukraine mwishoni mwa Februari ili kutetea wanaozungumza Kirusi katika mikoa ya mashariki ya Donetsk na Luhansk dhidi ya mateso ya utawala wa Kiev unaopata himaya ya madola ya Magharibu.

Aidha Russia imekuwa ikipinga hatua ya Ukraine ya kujikurubisha kwa muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi (NATO) ambao unaitazama Russia kama adui wake mkuu.

342/