Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

18 Novemba 2022

19:05:10
1324310

Kuongezeka mawazo ya kutaka kujiua miongoni mwa watoto na vijana wa Marekani

Matokeo ya utafiti uliofanya huko Marekani yanaonyesha kuwa mawazo na fikra za kutaka kujiua zimeongezeka sana kati ya watoto na vijana wa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, matokeo ya utafiti huo yaliyochapishwa katika jarida la matibabu la Pediatrics yanaonyesha kuwa idadi ya watu wanaolazimika kufika katika vituo vya matibabu vya Marekani imeongezeka kwa kasi kutokana na tabia ya watoto na vijana kutaka kujiua.

Kwa mujibu wa utafiti huo, idadi ya watoto na vijana waliofika katika vituo hivyo vya matibabu kushughulikiwa tatizo hilo iliongezeka kwa asilimia 59 kutoka mwaka wa masomo wa 2016-2017 hadi 2019-2020.

Ingawa janga la corona limeongeza mawazo ya kutaka kujiua miongoni mwa watoto na vijana wa Marekni katika miaka ya hivi karibuni, lakini utafiti unaonyesha kuwa tatizo hilo lilianza kabla ya janga la covid-19.

Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani pia ilitangaza Juni mwaka jana kwamba mzozo wa afya ya akili katika jamii ya nchi hiyo umeongezeka kwa njia ambayo haijawahi kushuhudiwa tena huko nyuma.

Ukubwa wa tatizo hilo unaonyesha kuwa jamii ya Marekani sio tu inakabiliwa na mgogoro wa afya ya akili, bali migogoro ya kijamii na kisiasa ambapo mabadiliko ya haraka ya kijamii pia yamekuwa na taathira kubwa zinazoathiri afya ya akili ya watu wa nchi hiyo na hasa tabaka la vijana.

Katika miaka michache iliyopita, kizazi cha vijana nchini Marekani kimekabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na janga la corona, vita, ukosefu wa usalama wa kifedha, kutumika silaha moto shuleni, mabadiliko ya hali ya hewa, migogoro ya kisiasa na kijamii na vurugu zinazosababishwa na ubaguzi wa rangi, kikabila na kijinsia. Hizo ni baadhi tu ya sababu ambazo zimepelekea kuongezeka msongo wa mawazo na nia ya kutaka kujiua katika kizazi kipya cha Marekani ikilinganishwa na vizazi vya zamani.

342/