Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

18 Novemba 2022

19:13:19
1324319

Yemen yalaani mauaji ya kijana Ali Atef huko Riyadh

Wizara ya Masuala ya Wageni ya Yemen imelaani mauaji yaliyofanywa na vyombo vya usalama vya Saudia dhidi ya raia wa nchi hiyo"Ali Atef Hazban Al-Ali" mjini Riyadh huku familia yake ikifichua maelezo ya kushtua ya tukio hilo.

Mtandao wa Al-Alam umeripoti kuwa, familia ya "Ali Atef Hazban Al-Ali" imethibitisha katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Sana'a kwamba mtoto wao wa kiume alitekwa nyara kutoka eneo lake la kazi mjini Riyadh mwezi Septemba mwaka huu, akapigwa kikatili na kisha kuuawa.

Familia hiyo imepinga madai yaliyotolewa na utawala wa Saudi Arabia kwamba sababu ya kifo cha Ali ni kukosa hewa.

Imesisitiza kuwa mamlaka ya Saudia haikuwaruhusu kuchunguza mwili wake, jambo linaloashiria kuhusika kwa vyombo vya usalama vya serikali ya Riyadh katika mauaji hayo.

Jinai ya utawala wa Saudia dhidi ya "Ali Atef Hezban Al-Ali" si ya kwanza kufanywa na utawala huo wa kifalme. Viongozi wa Saudi wana historia ndefu ya kuwaua kiholela raia wasio na hatia; na mtu mashuhuri zaidi aliyeuawa katika miaka ya karibuni kwa amri ya Mohammed bin Salman, mwana mfalme wa Saudi Arabia, alikuwa Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari mkosoaji wa utawala wa Kifalme wa nchi hiyo. Khashoggi aliuawa kwa kukatwa vipande vipande akiwa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia huko Istanbul nchini Uturuki.

Wakati huo huo Wizara ya Masuala ya Wageni ya Yemen imelaani vitisho vya askari usalama wa serikali ya Saudia kwa familia ya Al-Ali na jamaa zake ili kuwazuia kudai uchunguzi wa maiti au kupata ripoti juu kifo chake.

Vilevile imekosoa misimamo isiyo ya kibinadamu ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ikitoa wito kwa Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za binadamu kuwajibika kwa ukandamizaji unaofanywa na mamlaka ya Saudia dhidi ya raia wa Yemen wanaoishi katika nchi hiyo, na kuwapeleka wahusika mahakamani.

342/