Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

18 Novemba 2022

19:15:36
1324323

Wazayuni wapatwa na kiwewe cha kwenda Qatar wakati wa fainali za Kombe la Dunia

Utawala wa Kizayuni wa Israel umewaonya Wazayuni wasitembelee Qatar au wachukue tahadhari kubwa wakiweko nchini humo wakati wa fainali za Kombe la Dunia.

Fainali za kombe la dunia la kabumbu zitaanza nchini Qatar tarehe 20 mwezi huu Novemba na zitaendelea hadi tarehe 18 Disemba 2022. Hizi ni fainali za 22 za Kombe la Dunia na ni mara ya kwanza kufanyika katika nchi ya Kiarabu. 

Televisheni ya al Alam imetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, utawala wa Kizayuni unaoikalia kwa mabavu Quds Tukufu, umewataka mashabiki wa mpira wa utawala huo kutotembelea Qatar au kuchukua tahadhari sana kwani Qatar haiutambui rasmi utawala wa Kizayuni.

Utawala wa Kizayuni umetabiri kubwa, kati ya wakazi elfu 10 hadi 20 elfu wa ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina wataelekea Qatar kushuhudia kwa karibu fainali za Kombe la Dunia la mwaka huu.

Serikali ya Qatar imepiga marufuku safari za moja kwa moja za ndege kutoka Tel Aviv kuelekea mji mkuu wa nchi hiyo, Doha. Sasa hivi mashabiki hao wa kabumbu wa Israel hawajui hatima yao.

Mwanadiplomasia mmoja wa utawala wa Kizayuni amedai kuwa, iwapo Qatar itaruhusu Wazayuni kufika nchini humo, itakuwa na maana ya kutangaza uhusiano wake wa kawaida na utawala wa Kizayuni. Ingawa Qatar imelazimika kuwapa visa ya muda mashabiki hao, lakini imetangaza waziwazi kuwa hiyo haina maana ya kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni.

Fainali za Kombe la Dunia la mpira wa miguu kwa mwaka huu wa 2022 ambazo zitaanza Jumapili ijayo ya ya tarehe 20 Novemba zitafunguliwa kwa pambano baina ya wenyeji Qatar na timu ya taifa ya Ecuador. 

342/