Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

19 Novemba 2022

16:10:24
1324629

Kunyamazia mashambulio ya kigaidi yanayofanywa Iran hakuna tija nyingine isipokuwa kuimarisha ugaidi

Wizara ya Mambo ya Nje imetoa taarifa ambayo mbali na kulaani vitendo vya kigaidi katika miji ya Izeh, Esfahan na Mashhad imesisitiza kuwa: hakuna shaka kuwa kimya cha makusudi cha waenezaji fujo na machafuko ndani ya Iran wa kutokea nje ya nchi mbele ya hujuma zillizo dhahir shahir za kigaidi zilizofanywa katika miji kadhaa ya Iran, hakina matokeo mengine isipokuwa kuimarisha ugaidi ulimwenguni.

Mnamo Novemba 16, 2022, watu wawili waliokuwa wakiendesha pikipiki wakiwa na silaha za kivita waliwafyatulia risasi watu wa mji wa Izeh katika mkoa wa Khuzestan (kusini mwa Iran), wakawaua shahidi watu saba na kuwajeruhi wengine kumi.Katika shambulio jengine la kigaidi waendesha pikipiki wawili waliwashambulia walinda usalama huko Esfahan (katikati ya Iran) ambapo wanajeshi watatu wa vikosi vya usalama waliuawa shahidi na mwingine mmoja alijeruhiwa.Wanachama wa makundi ya kigaidi waliwaua shahidi pia walinzi wawili wa usalama wa jeshi la kujitolea la wananchi Basij katika mji wa Mashhad.Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, katika taarifa iliyotoa leo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeeleza kuwa: katika siku za hivi karibuni taifa tukufu la Iran na jamii ya kimataifa zimeshuhudia vitendo vya jinai vya kundi la magaidi makatili wasio na huruma dhidi ya raia wasio na hatia na walinzi wa usalama wa Iran katika miji ya Izeh, Esfahan na Mashhad.Katika taarifa yake hiyo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani vikali mashambulizi hayo maovu ya kigaidi na kutoa salamu za rambirambi kwa wananchi wote wa Iran hususan familia zilizofiwa za Mashahidi.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, maadui na wapinzani wa Mfumo mtakatifu wa Jamhuri ya Kiislamu na taifa tukufu na adhimu la Iran wanaficha sura na dhati yao halisi ya kijinai nyuma ya kizoro cha kinafiki cha kuwahurumia watu na watoto wa nchi hii.Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa yake kwamba, kwa mtazamo wa kanuni na taratibu za kimataifa, ugaidi wa aina yoyote na unaofanywa wakati na mahala popote pale unalaaniwa; hivyo ni wajibu wa jamii ya kimataifa na asasi za kimataifa kulaani vitendo vya kigaidi vya hivi karibuni nchini Iran na kutoruhusu kupatikana maficho salama kwa wanaoeneza machafuko na magenge ya misimamo ya kufurutu mpaka ambayo kuendelea kuishi kwao kunategemea uzushaji wao wa machafuko na uenezaji chuki, mivutano, fujo na uvurugaji amani.Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, kwa mujibu wa vigezo vya kimataifa na kulingana na sheria na kanuni zake, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itatumia haki yake kufuatilia kisheria vitendo vya kigaidi vinavyofanywa na magaidi pamoja na tawala zinazowaunga mkono.../


342/