Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

19 Novemba 2022

16:11:02
1324630

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Iran: Hatua za kinyama za kuwaua walinda amani hazitaachwa bila kujibiwa

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuhusu mauaji ya kinyama ya walinzi wawili wa amani katika mji wa Mashhad makao makuu ya mkoa wa Khorasani-Razavi, kaskazini mashariki ya nchi, kwamba hatua kama hizo zisizo za kiutu hazitaachwa bila kujibiwa.

Hujjatul-Islam Mohammad Jafar Montazeri, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Iran ameyasema hayo alipokagua sehemu wanakoshikiliwa baadhi ya wazusha machafuko na wavurugaji amani huko Mashhad na akaongeza kuwa: "adui amejitosa uwanjani kwa nguvu na uwezo wake wote, lakini taifa la Iran halihofu vitisho vyao na litazima hila za wazusha machafuko".Montazeri ameashiria njama zisizo na kikomo za adui za kuvuruga amani na usalama katika Iran ya Kiislamu, na akabainisha kuwa: "vitamseto, kamili na vya pande zote vimeanza dhidi ya wananchi wa Iran, lakini adui daima amekuwa akishindwa kutokana na ustahimilivu na uimara wa taifa hili kubwa; na mara hii pia atakatishwa tamaa ".Mwendesha Mashtaka Mkuuu wa Iran ameongeza kuwa: tangu muda mrefu nyuma adui alikuwa ameshapanga kuanzisha machafuko na kugawanya kazi za utekelezaji wake lakini wananchi waelewa na wenye basira wa Iran wamejitenga na njia ya maadui hao na jambo hilo limewafanya maadui waemewe na kukasirika.

Pamoja na kwamba kuzusha machafuko na kufanya mauaji ni moja ya mikakati inayotekelezwa kwa miaka kadhaa na maadui ikiwemo Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katika kukabiliana na Jamhuri ya Kiislamu, lakini katika wiki za hivi karibuni maadui hao wametumia uwezo wao wote wa kisiasa na wa vyombo vya habari kushadidisha manung'uniko, fujo na machafuko nchini Iran.

Siku ya Alhamisi jioni, katika eneo la makutano ya Hur Aamili mjini Mashhad, majambazi na wazusha machafuko kadhaa walitoa vitisho na kuwatia hofu wafanyabiashara ili wasifungue maduka yao katika eneo hilo, lakini mara baada ya kufika askari polisi na walinda amani wakatawanywa katika eneo hilo. Lakini baadhi ya wazusha machafuko hao waliwashambulia ghafla kwa visu vijana watano wa jeshi la kujitolea la wananchi Basij waliokuwa mbali na eneo la makabiliano na polisi, wakawaua shahidi wawili miongoni mwao na kuwajeruhi wengine watatu.../