Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

19:08:15
1325176

Uingereza yakiri, silaha zinazopelekwa Ukraine kutwaliwa na magaidi

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kitaifa wa Jinai nchini Uingereza (NCA) amesema silaha zinazopelekwa Ukraine na nchi za Magharibi yumkini zikafanyiwa magendo na kuishia mikononi mwa magenge ya wahalifu na magaidi katika kona mbalimbali za dunia.

Graeme Biggar amenukuliwa akisema hayo na gazeti la Sunday Times na kufafanua kuwa, "Katika mgogoro wowote ule, silaha zinapoingizwa kiwepesi (katika eneo la vita) ndivyo zinavyotoka kwa urahisi pia. Mwisho wa mgogoro, silaha za ziada zitatwaliwa na wahalifu na magaidi."

Biggar ameeleza bayana kuwa, licha ya vyombo vya usalama vya Ukraine kuwahakikishia kuwa silaha zote zilizotumwa nchini humo zipo katika mikono salama, lakini Polisi ya Ulaya (Europol) na taasisi nyingine za usalama za bara hilo zina wasi wasi kuwa huenda silaha hizo zikakosa kudhibitiwa.

Serikali ya Mocow inakadiria kuwa, silaha na zana za kivita zenye thamani ya dola bilioni moja za Marekani zinaingizwa nchini Ukraine kila mwezi, tangu vita baina ya nchi hiyo na Russia vianze mwezi Februari mwaka huu.

Magharibi inavyorundika silaha Ukraine

Uingereza imekiri kuhusu hatari ya silaha hizo zinazorundikwa Ukraine na nchi za Magharibi kuishia mikononi mwa magenge ya kigaidi katika hali ambayo, Wamagharibi si tu hawajachukua hatua za kuhitimisha vita huko Ukraine bali wameendelea kukoleza moto wa vita hivyo. 

Mapema mwezi uliopita, Konstantin Vorontsov, Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Kuzuia Uenezi na Udhibiti wa Silaha ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia alionya kuwa, misaada ya silaha ya Marekani kwa Ukraine itasababisha mzozo wa moja kwa moja wa kijeshi kati ya Russia na Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi (NATO). 

342/