Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

21 Novemba 2022

19:09:32
1325178

Taasisi ya "Democracy For The Arab World Now" yamkosoa Biden kwa kumpa kinga Bin Salman

Taasisi isiyo ya kiserikali ya "Democracy For The Arab World Now" imekosoa hatua ya Rais Joe Biden wa Marekani ya kumpatia kinga ya kutoshtakiwa mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman. Taasisi hiyo imeitaja hatua hiyo ya Biden kuwa ni natija ya siasa na sheria zisizo sahihi.

Mrithi huyo wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia ndiye aliyotoa amri ya kuuliwa mwandishi habari Jamal Khashoggi aliyekuwa akiukosoa pakubwa utawala wa Aal Saud. Khashoggi aliuawa na maajenti wa Saudi Arabia Oktoba Pili mwaka 2018 mara bada ya kuwasili katika ubalozi mdogo wa Saudia huko Istanbul Uturuki.  

Taasisi isiyo ya kiserikali ya "Democracy For The Arab World Now" imetoa taarina na kutangaza kuwa, hatua ya serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani ya kumtambua rasmi Mohammed bin Salman mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia kama Waziri Mkuu wa Saudi Arabia inaamanisha kumpa kinga ya kutoshtakiwa dhidi ya mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya Jamal Khashoggi mwandishi habari mtajika aliyekuwa akiukosoa sana utawala wa Aal Saud. Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali imekitaja kitendo hicho cha Rais wa Marekani kuwa ni kosa kwa upande wa kisheria na kisera. 

Kesi iliyowalishwa na Taasisi ya Democracy For The Arab World Now na mke wa mwendazake Jamal Khashoggi kwa jina la Khadija Cengiz katika mahakama ya shirikisho nchini Marekani kwa mujibu wa sheria za shirikisho na kimajimbo za nchini Marekani imejaribu kumuarifisha Mohammed bin Salman na watuhumiwa wengine 20 kuwa wamehusika  katika mauaji hayo.  

Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali kwa ajili ya Ulimwengu wa Kiarabu imeongeza kuwa, uamuzi wa kumpatika kinga bin Salman ulikuwa ni hila mbaya na ya dhahiri; na lengo lake halikuwa ni kumuongezea nafasi muhimu katika majukumu yake  mrithi huyo wa kiti cha ufalme wa Saudia, bali lengo kuu lilikuwa ni kumpatia kinga ya kisheria ili asishtakiwe.  

342/