Main Title

source : Parstoday
Jumatano

23 Novemba 2022

17:09:17
1325681

Yemen: Zaidi ya watoto elfu 4 wa Yemen wameuawa katika mashambulizi ya muungano wa Saudia

Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imetangaza kuwa zaidi ya watoto elfu 4 wa Yemen wameuawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya muungano vamizi unaoongozwa Saudi Arabia.

Shirika la kisheria linalofuatilia matukio yanayohusiana na watoto wa Yemen limetangaza katika ripoti yake kuwa watoto elfu 4 na 17 wameuawa na wengine 4,588 wamejeruhiwa katika mashambulizi ya muungano vamizi wa Saudia katika kipindi cha miaka 8 iliyopita.

Kwa upande mwingine, Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen imeashiria kwamba ripoti hiyo imenthibitisha jinai zinazohusiana na muungano vamizi na kuongeza kuwa: Hali hiyo ni chungu na mbaya zaidi kwa watoto wadogo.

"Abd al-Wahhab al-Mahbashi, mjumbe wa Ofisi ya Kisiasa ya Serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen, amebainisha kuwa historia haijawahi kuona jinai mbaya zaidi kuliko zile zinazofanywa na muungano vamizi unaoongozwa na Saudia na Marekani dhidi ya watu wa Yemen na ameongeza kuwa Wayemeni hawatasahau mauaji ya watoto wao na wanawake na watalipiza kisasi uhalifu unaofanywa dhidi ya watu wa nchi hiyo.

Hapo awali shirika la kutetea haki za binadamu la Intisaf lilitangaza kuwa, watoto elfu nane na 116 wa Yemen wameuawa au kujeruhiwa tangu kuanza uvamizi wa Saudia na Marekani nchini humo.

Maelfu ya watoto wa Yemen wameuawa katika mashambulizi ya Saudia

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika hilo la kutetea haki za binadamu, takriban raia 6,000 wa Yemen wamepata ulemavu kutokana na mashambulizi ya muungano wa Saudia, na kwamba 5,559 miongoni mwao ni watoto.

Ripoti hiyo inasema: Watoto milioni 2 laki 4 kati ya watoto wapatao milioni 10 walio na umri wa kwenda shule wa Yemen wamekosa elimu. Imeongeza kuwa, kutokana na mzingiro wa pande zote wa Saudia na washirika wake dhidi ya watu wa Yemen, watoto milioni 2 laki 3 wenye umri wa chini ya miaka mitano wa Yemen wanasumbliwa na utapiamlo.

342/