Main Title

source : Parstoday
Alhamisi

24 Novemba 2022

19:48:59
1325946

Al Sudani afanya mazungumzo na mrithi wa kiti cha ufalme wa Kuwait

Waziri Mkuu wa Iraq amekutana na kufanya mazungumzo na mrithi wa kiti cha ufalme wa Kuwait na kusisitiza juu ya ulazima wa kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili.

Waziri Mkuu wa Iraq Mohammad Shia Al Sudani pamoja na ujumbe wake alioambatana nao huko Kuwait jana Jumatano walilakiwa katika ikulu ya al Bayan nchini humo na mrithi wa kiti cha ufalme wa Kuwait, Sheikh Mishal Al Ahmad al Jaber al Sabah na Waziri Mkuu wa Kuwait Sheikh Ahmad Nawaf al Ahmad al Sabah.

Akiwa katika ziara rasmi nchini Kuwait, Waziri Mkuu wa Iraq Mohammad Shia Al Sudani amekuwa na mazungumzo na Sheikh Mishal Al Ahmad al Jaber al Sabah mrithi wa kiti cha ufalme wa nchi hiyo ambapo pande mbili hizo zimebadilisha mawazo kuhusu uhusiano wa nchi mbili na matukio ya kikanda na kimataifa. 

Al Sudani amesisitiza ulazima wa kuimarisha uhusiano  na ushirikiano kati ya nchi mbili hizo katika nyanja zote. 

Waziri Mkuu wa Iraq ameeleza kuwa: Iraq inataka kuwa na uhusiano wenye mlingano kati yake na jirani yeke huyo kwa mujibu wa kuheshimiana pande mbili na kulinda mamlaka ya kujitawala nchi mbil. Aidha amesema, Baghdad inafanya juhudi ili kutatua masuala mengi yanayozihusu nchi mbili za Kuwait na Iraq kwa mujibu wa maslahi ya pamoja na kwa lengo la kudumisha amani na uthabiti katika eneo.  

Katika mazungumzo hayo, Al Ahmad al Sabah pia amesifu uhusiano mwema kati ya nchi mbili hizo na nafasi muhimu ya Iraq katika eneo na jitihada zinazofanywa na nchi hiyo ili kuimarisha usalama wa kudumu Mashariki ya Kati; na kusisitiza kuwa, Kuwait inaunga mkono hali ya uthabiti huko Iraq.  

342/