Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

25 Novemba 2022

18:01:36
1326142

ILO: Wahajiri zaidi ya 50,000 wamefariki, utambulisho wa 30,000 haujaweza kufahamika

Ripoti mpya ya Shirika la Kimataifa la Uhajiri, ILO inaonyesha kuwa zaidi ya watu 50,000 wamepoteza maisha katika njia mbalimbali walizotumia kwa ajili ya kuhajiri kuelekea ughaibuni katika kipindi cha miaka minane iliyopita.

Julia Black, ripota wa Shirika la Kimataifa la Uhajiri, ameeleza kuwa, tangu ilipoanza "Kampeni ya Wahajiri Waliotoweka" mnamo mwaka 2014 na licha ya kuongezeka idadi ya watu wanaofariki dunia katika hekaheka za uhajiri, serikali zimechukua hatua chache za kuchunguza na kushughulikia maafa ya kimataifa ya wahajiri wanaotoweka bila kujulikana hatima yao. Ripota huyo wa Shirika la Kimataifa la Uhajiri ameongeza kuwa: wakati maelfu ya vifo vinavyotokea katika njia zinazotumiwa na wahajiri vinasajiliwa kila mwaka, ni hatua chache sana zimechukuliwa kuchunguza madhara yanayosababishwa na majanga hayo, seuze kuyazuia!Kulingana na ripoti hiyo ya ripota wa ILO, utambulisho na utaifa wa zaidi ya wakimbizi 30,000 waliopoteza maisha haujaweza kufahamika.

Miongoni mwa wahamiaji waliotoweka ambao utaifa wao umeweza kutambuliwa, kuna zaidi ya watu 9,000 kutoka nchi za Afrika, zaidi ya watu 6,500 kutoka Asia na watu 3,000 kutoka bara la Amerika.Afghanistan, Syria na Myanmar zimetajwa kuwa ndizo nchi tatu kuu wanakotoka wakimbizi na imeelezwa kuwa ukatili na hali isiyoridhisha ya ndani katika nchi ndizo sababu zinazowafanya raia wengi wa nchi hizo waamue kuhama makwao.../

342/