Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

26 Novemba 2022

18:34:48
1326425

Wauguzi wa Uingereza kufanya mgomo mwezi ujao kudai malipo bora

Wauguzi kote nchini Uingereza mwezi ujao watafanya mgomo ambao pamoja na mambo mengine unadai malipo bora.

Mgomo huo ambao utakuwa wa kwanza katika historia ya miaka 106 ya chama chao cha wauguzi unatarajiwa kujumuisha wafanyakazi wengine wa Uingereza kuchukua hatua za kusimamisha kazi wakidai malipo bora.

Wafanyakazi nchini Uingereza, Wales na Ireland ya Kaskazini  watafanya mgomo tarehe 15 na tarehe 20 Disemba mwezi ujao, baada ya chama chao cha Royal College Nursing ( RCN) kusema kwamba, serikali imekataa kuweko mazungumzo baina ya pande mbili kwa minajili ya kusikiliza malalamiko yao.

Hii itakuwa hatua ya hivi karibuni ya kusimamisha kazi nchini Uingereza ambapo mzozo wa miongo kadhaa wa mfumuko mkubwa wa bei na gharama kubwa ya maisha, umepelekea wafanyakazi katika sekta mbalimbali kudai nyongeza ya mishahara ili kumudu kupanda kwa bei za bidhaa za msingi. 

Mkurungenzi wa chama hicho cha wauguzi (RNC) Patricia Marquis amewaomba radhi wagonjwa ambao wangefanyiwa upasuaji au matibabu, na kusema kuwa “ wauguzi wamesimama ili kutetea haki zao, lakini muhimu zaidi kutetea haki za wagonjwa.”

Tayari kumeibuka wasiwasi mkubwa miongoni mwa raia wa Uingereza baada ya tangazo hilo la kuitishwa mgomo wa wauguzi mwezii ujao.

Mgomo huo unatarajiwa kuathiri pakubwa sekta ya afya nchini Uingereza. Miito mbalimbali imeanza kutokea inayoitaka serikali ya London kuitisha kikao cha mazungumzo na wauguzi hao kabla ya kkuwadia tarehe ya mgomo iliyotangazwa na chama cha wauguzi katika nchi hiyo ya bara Ulaya.

342/