Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

26 Novemba 2022

18:38:31
1326431

Walowezi wa Kizayuni wachoma moto magari ya Wapalestina katika mji wa Quds

Walowezi wa Kizayuni wameendelea kufanya vitendo vyao vya kinyama dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina ambapo wamechoma moto magari kadhaa ya Wapalestina katika mji wa Quds.

Vitendo hivyo vya kinyama ambavyo vimeongezeka mno katika miezi na majuma ya hivi karibuni jana vilishuhudiwa tena baada ya vitongoji kadhaa vya mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu kushuhudia matukio ya kuchomwa moto magari ya Wapalestina.

Taarifa zaidi zinasema kuwa, magari manne ya Wapalestina yamechomwa moto na kuteketea kikamilifu katika kitongoji cha Abu Ghosh kaskazini magharibi mwa mji wa Quds unaokaliwa kwa mabavu,

Tukio jingine kama hilo limetokea katika kitongoji cha Ein Naqquba kilichoko magharibi mwa mji huo ambapo magari mengine manne pia ya Wapalestina yamechomwa moto.

Kadhalika walowezi hao wa Kizayuni wameandika ibara na maneno ya kibaguzi katikka kuta za nyumba za Wapalestina katika vijiji hivyo viwili. 

Hili siyo tukio la kwanza, bali matukio kama haya yamekuwa yakishuhudiwa mara kwa mara katika maeneo ya Wapalestina yanayokaliwa kwa mabavu ambapo walowezi hao wamekuwa wakipata himaya na uungaji mkono kikamilifu kutoka kwa vyombo vya usalama vya utawala haramu wa Israel.

Hayo yanaripotiiwa katika hali ambayo, katika miezi ya hivi karibuni vitendo vya hujuma na uvamizi wa walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina hususan katika Msikiti wa al-Aqswa vimeongezeka mno.

Asasi za kimataifa kama Umoja wa Mataifa na baraza lake la usalama zinakosolewa na kulaumiwa kutokana na kutochukua hatua za maana za kukabiliana na hatua mbalimbali zisizo za kibinadamu zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel huko Palestina. 

342/