Main Title

source : Parstoday
Jumapili

27 Novemba 2022

16:46:50
1326731

Wizara ya Ulinzi ya Russia: Wamarekani wametengeneza virusi vipya vya corona

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa: Chuo Kikuu cha Boston cha nchini Marekani kimetengeneza virusi vipya aina ya Omicron vinavyosababisha ugonjwa wa Corona.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Russia imeongeza kuwa, kwa mujibu wa aina ya Omicron na virusi vya awali kabisa vilivyogunduliwa huko Wuhan China, Chuo Kikuu cha Boston cha nchini Marekani kimezalisha virusi vipya ambavyo husababisha ugonjwa wa corona. 

Taarifa hiyo imeendelea kubainisha kuwa, virusi hivyo vilivyobadilishwa vimesababisha asilimia 80 ya vifo kwa sampuli za wanyama zilizofanyiwa majaribio na  kusababisha dalili zisizo za kawaida katika neva na uharibifu mkubwa wa mapafu.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Russia imebainisha kuwa: majaribio ya kinga ya mwili yaliyofanywa kwa wanyama hao  yameonyesha kupungua mara 11 kwa uwezo wao wa mwili wa kukabiliana na vimelea vya maradhi  na kutofanya kazi kwa chanjo zilizopo.

342/