Main Title

source : Parstoday
Jumanne

29 Novemba 2022

18:44:14
1327326

Balozi wa Afrika Kusini akosoa vikwazo vya madola ya Magharibi dhidi ya Iran

Balozi wa Afrika Kusini nchini Iran amekosoa kuendelea vikwazo vya madola ya Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Vika Mazwi Khumalo Balozi wa Afrika Kusini nchini Iran ameyasema hayo Jumatatu wakati alipotembelea kituo cha kuzalisha umeme aina ya CCP chenye uwezo wa kuzalisha megawati 460 katika mkoa wa Mazandaran  kaskazini mwa Iran na kuongeza kuwa: "Vikwazo vya Magharibi dhidi ya Iran vimezuia kupanuka kwa miamala ya biashara na benki kati ya Jamhuri ya Kiislamu na nchi nyingine."

Kumalo amebaini kuwa: "Kwa kuwa makampuni mengi ya Afrika Kusini yapo katika sekta binafsi na yana mabadilishano ya kibiashara na nchi za Magharibi, iwapo yatawasiliana na Iran, uhusiano wao na nchi nyingine utakatika, hivyo yanajizuia zaidi kupanua ushirikiano na Iran.

Mwanadiplomasia huyu wa Afrika Kusini alisema: Hadi sasa hati 23 za maelewano zimetiwa saini kati ya Afrika Kusini na Iran, na 18 kati yake zimetekelezwa, na hati nyingine za maelewano zitachunguzwa katika tume ya pamoja ya nchi hizo mbili itakayofanyika mwaka ujao."

Balozi wa Afrika Kusini nchini Iran amesema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo tofauti katika anuai ya sekta na Afrika Kusini iko tayari kupanua uhusiano wa kibiashara na Iran hususan wafanyabiashara wa mkoa wa Mazandaran.

342/