Main Title

source : Parstoday
Jumanne

29 Novemba 2022

18:46:00
1327329

Rais wa Algeria: Kuiunga mkono Palestina kusiishie kwenye utoaji taarifa tu

Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amesisitiza haja ya kuchukuliwa hatua za kivitendo ili kurejesha haki za Wapalestina.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, Tebboune, amezitaka nchi duniani kuchukua hatua za kivitendo za kuunga mkono haki za watu wa Palestina na akaeleza kwamba uungaji mkono huo haupasi kujifunga na utoaji msururu wa kauli na taarifa tu.Rais wa Algeria ameendelea kusisitiza kwa kusema: "sisi nchi za Kiarabu inatupasa turejeshe moyo wetu wa kujiamini ili tuweze kuwa na taathira katika upeo wa kimataifa. Inapasa sisi sote kwa pamoja tuunde kambi imara ya kiuchumi".

Katika hotuba aliyotoa kitambo nyuma, Rais wa Algeria alitilia mkazo umuhimu wa kuliunga mkono taifa la Palestina na akasema: "piganio tukufu la taifa la Palestina litabaki kuwa kadhia kuu, mhimili mkuu na suala la msingi kwetu, ambalo linalengwa kufutwa na maghasibu (wa Kizayuni) kupitia hatua wanazochukua".

Algeria imekuwa mtetezi wa haki za wananchi wa Palestina tangu mwanzoni mwa kadhia ya Palestina na imekuwa ikiunga mkono piganio tukufu la ukombozi wa Quds kwa njia mbalimbali.Haki za wananchi madhulumu wa Palestina zinaendelea kukanyagwa na kuporwa na utawala ghasibu wa Kizayuni na kwa jinai unazoendelea kufanya kwa zaidi ya miaka sabini sasa.../


342/