Main Title

source : Parstoday
Jumatano

30 Novemba 2022

21:08:45
1327603

Sensa Uingereza: Idadi ya Waislamu yaongezeka; Wakristo wazidi kupungua

Idadi ya Waislamu inazidi kuongezeka kwa kasi nchini Uingereza huku wafuasi wa dini ya Kikristo ikipungua katika taifa hilo la bara Ulaya.

Takwimu za sensa ya makazi na watu zinaonyesha kuporomoka kwa idadi ya Wakristo nchini Uingereza na kwamba, chini ya nusu ya idadi ya watu England na Wales ni Wakristo.

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa jana Jumanne sensa ya kipindi cha miaka 10 iliyofanywa mwaka jana 2021 inaonesha ongezeko kubwa la watu wenye kufuata dini ya Kiislamu, wakifuatiwa na watu wasiokuwa na dini.

Takwimu hizo zimetolewa na ofisi ya taifa ya Tawimu ONS. Moja ya maswali yaliyoulizwa katika zoezi hilo la kuhesabu watu ni kuhusu dini na ambalo kimsingi liliorodheshwa katika utafiti huo tangu mwaka 2001 likiwa ni swali la hiari.

Askofu wa York, Stephen Cottrell amesema matokeo hayo hayashangazi sana kuona idadi ya Wakristo imekuwa ikiporomoka kadiri muda unavyokwenda, ingawa ameeleza kuwa, kutokana na mgogoro wa ughali wa maisha na vita barani Ulaya, watu bado wanahitaji kuendelea kushikilia imani ya kiroho. Wakristo wanakadiriwa kuwa, kiasi milioni 27.5 England na Wales idadi ambayo inaonesha imeshuka kwa asilimia 13.1 kutoka mwaka 2011. Idadi ya aislamu imeongezeka kutoka asilimia 4.9 hadi asilimia 6.5. 

Idadi ya Waislamu nchini Uingereza na mataifa mengine barani Ulaya inazidi kuongezeka licha ya chuki na propaganda chafu zinazoenezwa na makundi ya kufurutu ada dhidi ya dini ya Kiislamu.

Mashirika ya kiraia ya Kiislamu yamekuwa yakizishutumu nchi za Ulaya hasa Uingereza, Denmark, Ufaransa na Austria kwa kukandamiza jamii za Kiislamu, na hivyo kuzusha hali ya wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa wimbi la chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) inayofadhiliwa na serikali barani Ulaya.

342/