Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

3 Desemba 2022

15:59:51
1328255

Wapiganaji zaidi ya 40 wa Boko Haram waangamizwa Nigeria

Mkurugenzi wa Idara ya Habari ya Wizara ya Ulinzi ya Nigeria ametangaza mapema leo Jumamosi kwamba magaidi 44 wa kundi la Boko Haram wameuawa katika operesheni za anga na nchi kavu za jeshi kaskazini mwa nchi hiyo.

Brig.-Gen Musa Danmadami ametangaza kuwa magaidi hao 44 wa Boko Haram waliuawa wiki iliyopita katika operesheni za jeshi la Nigeria katika mkoa wa Borno.

Ameongeza kuwa: Vikosi vya jeshi pia viliwakamata magaidi wengine 47 wakati wa operesheni hiyo na vimefanikiwa kuwakomboa mateka 10 kutoka kwa magaidi hao.

Kundi la kigaidi la Boko Haram lilishika silaha mwaka 2009 kwa lengo la kujiimarisha kaskazini mwa Nigeria na baadaye lilipanua mashambulizi yake katika nchi za Niger, Chad na kaskazini mwa Cameroon.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu imetangaza kuwa, zaidi ya watu elfu 30 wameuawa na karibu watu milioni tatu wamelazimika kukimbia makazi yao kutokana na harakati za kigaidi za Boko Haram katika muongo mmoja.

342/