Main Title

source : Parstoday
Jumatano

7 Desemba 2022

19:36:50
1329391

ICC yatakiwa kuzipatia kipaumbele jinai zinazojiri mashariki mwa Kongo

Waziri wa Sheria wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amemtaka Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya ICC kuchunguza mauaji ya halaiki yaliyojiri wiki jana katika mji wa Kishishe mashariki mwa Kongo.

Bi Rose Mutombo amesema hayo katika kikao cha 21 cha Bunge la Nchi Wanachama kwenye Mkataba wa Roma wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC). 

Waziri wa Sheria wa Kongo amesema kwamba: "Tukiwa kwenye chumba hiki hivi sasa,  eneo la mashariki mwa nchi yangu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo katika mikoa ya Ituri na Kivu ya Kaskazini kuunatendeka jinai dhidi ya binadamu, jinai za kivita, jinai za mauaji ya kimbari na jinai za ukandamizaji ambazo zimesababisha maelfu ya vifo na pia kesi ya udhalilishaji wa kingono hususan dhidi ya wanawake na wasichana mbali na idadi kubwa ya watu waliohama makazi yao." 

Shirika la habari la taifa la Kongo limeripoti kuwa, Waziri wa Sheria wa nchi hiyo Rose Mutombo ameyanyooshea kidole cha lawama makundi ya kigaidi ya ADF kutoka Uganda na waasi wa kundi la M23 wanaoungwa mkono na Rwanda na kuwataja kuwa wanahusika na jinai hizo.

Serikali ya Kinshasa inawatuhumu waasi wa M23 kuwa ndio waliokishambulia kijiji cha Kishishe yapata umbali wa kilomita 70 kutoka mji wa Goma na kuuwa watu zaidi ya 200. Jumatatu wiki hii msemaji wa serikali ya Kongo, Patrick Muyaya, alisema wataanzisha uchunguzi rasmi  kuhusu hujuma iliyotekelezwa huko Kishishe katika jimbo lenye machafuko la Kivu Kaskazini; mashambulizi ambayo yamevunja mapatano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwezi uliopita. 


342/