Main Title

source : Parstoday
Jumatano

7 Desemba 2022

19:37:39
1329392

Waziri wa Usalama Marekani aeleza wasiwasi wake juu ya vurugu na machafuko ya ndani

Waziri wa Usalama wa Nchi wa Marekani ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na ukatili na machafuko ya ndani akivitaja kuwa ni moja ya vitisho vikubwa vinavyofungamana na ugaidi wa ndani ya nchi hiyo.

Matokeo ya uchunguzi wa mashirika ya kisheria na taasisi za utekelezaji wa sheria yaliyotolewa katikati ya mwaka huu wa 2022 yanaonyesha kuwa uhalifu wa kikatili unaongezeka nchini Marekani licha ya kupungua kwa mauaji katika baadhi ya miji mikubwa ya nchi hiyo.

Matokeo ya uchunguzi huo yaliyochapishwa na vyombo vya habari vya Marekani yanaonesha kuwa, kiwango cha uhalifu wa kikatili hakijarudi katika kiwango cha kabla ya maambukizi ya Corona, na kwamba ingawa visa vya mauaji na ubakaji vinaonekana kupungua katika miji kadhaa lakini suala hilo halijumuishi miji yote, bali kinyume chake, jinai na ukatili unaonekana kuongezeka katika baadhi ya miji ya nchi hiyo. 

Kulingana na matokeo ya utafiti huo, uhalifu wa vitendo vya kikatili uliongezeka kwa asilimia 4.2 mnamo Januari hadi Juni 2022 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Waziri wa Usalama wa Nchi wa Marekani, Alejandro Mayorkas, amesema kuwa: "Tunakabiliwa na wimbi linaloongezeka la changamoto za ugaidi, ndani ya nchi na ulimwenguni kote."

Mallorcas ameongeza kuwa: "Uchupaji mipaka na ukatili wa ndani ni miongoni mwa vitisho vikubwa vyenye mfungamano na ugaidi nchini Marekani."

342/