Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

17 Desemba 2022

21:08:43
1331610

Umoja wa Mataifa wazindua muongo wa lugha za asili

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limezindua Muongo wa Lugha za Jamii ya Asili, katika kikao kilichoitishwa na Rais wa Baraza hilo, Csaba Kőrösi.

Akifungua mkutano huo, Kőrösi amesema lugha ni msingi muhimu katika ufahamu hali kadhalika katika utambulisho wa kila jamii.

Hata hivyo amesema kadri lugha za jamii ya asili zinavyotoweka,  ndivyo unavyotoweka utamaduni, mila na ufahamu ambao lugha hizo zimebeba.

Ametoa wito kwa nchi wanachama kushirikiana na jamii za watu wa asili ili kuchukua hatua kuu tatu.

Hatua hizo ni mosi; kulinda haki za watu wa jamii ya asili, kama vile elimu kupitia lugha zao mama. Pili; kuhakikisha watu wa jamii ya asili na ufahamu walio nao wa kiasili havitumiki vibaya na wapatiwe taarifa ya awali pindi watu wanapotaka kutumia ufahamu au lugha zao. Tatu; kushauriana na watu wa jamii ya asili, kuwashirikisha katika kila mchakato wa maamuzi yanayowahusu.

342/