Main Title

source : Parstoday
Jumanne

3 Januari 2023

16:38:30
1335744

Nyumba 200 zateketezwa kwa moto nchini Afrika Kusini

Moto mkubwa uliotokea katika kitongoji duni nje kidogo ya mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini umeua mwanamke mmoja na kuharibu zaidi ya nyumba 200.

Tukio hilo la moto lilitukia mapema usiku wa kuamkia jana Jumatatu katika eneo la makazi duni la Philippi viungani mwa Cape Town.

msemaji wa shirika la misaada ya kibinadamu la Gift of the Givers, Ali Sablay amesema: "Zaidi ya majengo 300 yameteketea na kwamba takriban watu 1,000 waliachwa bila makazi na mwanamke mmoja amefariki dunia."

Msemaji wa Idara ya Zimamoto eneo hilo mesema: Tukio hilo liliripotiwa saa 8:40 usiku wa kiamkia jana Jumatatu, na kwamba mwanamke ambaye aliungua vibaya alifariki duinia kutokana na ukali wa majeraha yake.

Aliongeza kuwa: "Chanzo halisi cha moto huo kilikuwa bado hakijajulikana, lakini shahidi aliyekuwepo eneo hilo amedai kuwa moto huo ulianzia kwenye nyumba ya mwanamke aliyeaga dunia."

Kwa mujibu wa afisa huyu wa Idara ya Zimamoto ya Afrika Kusini, moto huo ulianza baada ya jiko la gesi la nyumba ya mama huyo kushika moto na ulienea kwa kasi kubwa kutokana na upepo mkali na kuteketeza zaidi ya nyumba 200 za kitongoji hicho.

Watu wengi ambao nyumba zao zimeteketea kwa moto walikuwa safarini katika likizo ya mwaka mpya.

342/