Main Title

source : Parstoday
Jumatano

11 Januari 2023

16:59:26
1337783

Hizbullah yailaani Charlie Hebdo kwa kumvunjia heshima Kiongozi Muadhamu

Harakati ya muqawama ya Hizbullah ya Lebanon imelaani vikali kitendo cha jarida la Ufaransa la Charlie Hebdo cha kumvunjia heshima Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Taarifa ya Hizbullah imeitaka serikali ya Ufaransa kuchukua hatua na kuwaadhibu waliohusika na kitendo hicho kiovu cha kuchapisha picha za kuudhi zilizoandamana na maneno na misemo michafu na ya matusi dhidi ya Kiongozi Muadhamu.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, "Serikali ya Ufaransa haipaswi kuwa sehemu ya jinai hii, iwachukulie hatua madhubuti waliofanya kitendo cha kuwakejeli viongozi wahashamu wa taifa (la Iran)."

Harakati hiyo ya muqawama ya Lebanon imeeleza bayana kuwa, uafriti huo wa jarida la Kifaransa la Charlie Hebdo haupasi kupita hivi hivi bila ya kupatiwa jibu muafaka.

Katika toleo lake maalumu la Jumatano iliyopita ya Januari 4, jarida hilo la Ufaransa lilifanya kitendo cha kipuuzi cha kuanzisha shindano la kimataifa la michoro na vibonzo, ambapo lilichapisha picha za kuudhi zilizoandamana na maneno, misemo michafu na ya matusi dhidi ya viongozi wa dini. 

Viongozi wa Iran wamekosoa hatua ya jarida hilo la Ufaransa ya kukashifu na kuvunjia heshima wanazuoni, matukufu na thamani za kidini na kitaifa za Jamhuri ya Kiislamu. Balozi wa Ufaransa mjini Tehran aliitwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran kubainishwa malalamiko hayo ya Jamhuri ya Kiislamu.

342/