Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

13 Januari 2023

15:14:29
1338089

Trump alipendekeza Marekani iishambulie Korea Kaskazini kwa silaha za nyuklia

Donald Trump alipendekeza wakati wa utawala wake katika mkutano na wasaidizi wake, Marekani iishambulie Korea Kaskazini kwa silaha za nyuklia.

Kwa mujibu wa televisheni ya Sky News, mwandishi wa gazeti la New York Times Michael Schmidt ameeleza katika sura mpya ya kitabu chake kiitwacho "Donald Trump dhidi ya Marekani"  (Donald Trump vs The United States) ​​alichokichapisha kwa mara ya kwanza mwaka 2020 ya kwamba: mnamo 2017, katika mwaka wa kwanza wa urais wake, Trump alipendekeza katika mkutano na wasaidizi wake, Marekani iishambulie Korea Kaskazini kwa silaha za nyuklia na akatangaza kuwa, Washington inaweza kuitaja nchi nyingine kwamba ndio iliyohusika na shambulio hilo.Mnamo Agosti mwaka huo, Trump alimtahadharisha Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un kuhusu kitisho cha Marekani kwa kumwambia "Korea Kaskazini itakabiliwa na moto na ghadhabu ambao ulimwengu haujawahi kuona mfano wake".

Marekani na wajumbe wenzake wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wameiwekea vikwazo mara kadhaa Korea Kaskazini tangu ilipofanya jaribio lake la kwanza la nyuklia mwaka 2006.

Itakumbukwa kuwa, ili kutatua mzozo baina ya nchi yake na Marekani, mwaka 2018 kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un alikutana mara mbili na Rais wa wakati huo wa Marekani Donald Trump katika nchi za Singapore na Vietnam, lakini mikutano yao haikuzaa matunda; na baada ya hapo, Marekani ikashadidisha mashinikizo ya kiuchumi dhidi ya Korea Kaskazini na kuiwekea vikwazo zaidi nchi hiyo.
Kwa upande wake na ili kukabiliana na vitisho vya Washington, Pyongyang ikachukua hatua zaidi za kuimarisha na kustawisha mpango wake wa makombora.Korea Kaskazini imeshasisitiza kuwa haitasitisha mpango wake wa uundaji makombora na silaha za nyuklia hadi Marekani itakapokomesha sera yake ya kiuadui na kiuhasama dhidi yake.../


342/