Main Title

source : Parstoday
Jumanne

31 Januari 2023

15:52:26
1342714

Erdogan: Uhusiano wangu na Putin ni wa "ukweli na kuaminiana"; Macron "si mkweli"

Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki amesema, uhusiano wake na Rais Vladimir Putin wa Russia na kwa ujumla kati ya nchi hizo mbili ni wa "ukweli na wenye msingi wa kuaminiana" na akamtaja Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa kuwa "si mtu mkweli".

Erdoğan ameyasema hayo katika mkutano na vijana wa Uturuki ambao umerushwa hewani na televisheni ya TRT na akaongezea kwa kusema: "katika uhusiano na Russia tunaheshimiana na kuaminiana", na akafafanua kuwa, uhusiano wake na Putin unatokana na kuwepo ukweli na nia safi, na kwamba matakwa yote ya Uturuki kuhusu maeneo ya Tatarstan na Dagestan yametekelezwa.Kwa mujibu wa rais wa Uturuki, kumekuwa na kile alichokiita "vitisho vingi" kutoka nchi zingine kuhusiana na ununuzi wa mitambo ya Russia ya S-400, lakini Uturuki imeinunua mifumo hiyo ya makombora na inayo hivi sasa.Katika muktadha huo huo, Erdogan ameashiria suala la uwezekano wa nchi yake kupatiwa ndege za kivita aina ya F-16 na F-35 na akasema kuihutubu Marekani: "kuhusu ndege za F-16 tunataka tuzipate kutoka kwenu (Marekani), lakini mumehalifu ahadi zenu".

Katika mkutano huo Erdoğan amejibu pia suali kuhusu mwaliko aliotoa hapo awali kwa Ufaransa wa kuhudhuria mkutano wa "Jumuiya ya Nchi Zinazozungumza Kituruki", na akaashiria namna rais Emmanuel Macron wa Ufaransa asivyo mkweli kwa kusema: "tunataka siasa za kimataifa ziendane na ukweli, pasipo na ukweli hakuna heshima".

Rais wa Uturuki ameongeza kuwa, "Ufaransa inapoteza kwa kasi itibari na uaminifu wake, na hivi sasa yeye (Macron) amepoteza uaminifu wake katika Bunge la Ufaransa, na Paris ingali inaendelea kupoteza itibari yake".../


342/