Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

3 Februari 2023

12:44:24
1343310

Iran yakosoa mtazamo wa nchi za Magharibi kuhusu haki za binadamu

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amekosoa mtazamo wa nchi za Magharibi kuhusu haki za binadamu kwa kuchapisha picha za mashahidi wa Kipalestina waliouawa na jeshi la Israel katika mwezi uliopita.

Nasser Kan'ani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran mapema leo Alkhamisi amechapisha picha za mashahidi wa Kipalestina waliouawa na Israel katika mwezi uliopita kwenye ukurawa wake wa Twitter na kuandika: Mwezi Januari Wapalestina 35 waliuawa shahidi na utawala wa Kizayuni katika maeneo tofauti ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Huu ndio mtazamo mwingine wa uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa haki za binadamu!

Akiashiria matukio ya hivi karibuni katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba: Kutoweka na kuangamia kunaambatana na asili ya utawala wa Kizayuni.

Nasser Kan'ani ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: Hatua za uharibifu za utawala wa Kizayuni dhidi ya mhimili wa muqawama hazitauzuia utawala huo kusambaratika. 

Kan'ani ameongeza kuwa, kwa utawala unaokumbwa na migogoro mikubwa ya ndani na unaokabiliwa na mapambano ya wapigania uhuru na ukombozi wa Palestina katika maeneo 3 ya Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na ardhi 1948, kujihusisha na vitendo vya maudhi dhidi ya Mhimili wa Muqawama hakutauokoa utawala huo haramu.  

Umepita mwezi mmoja sasa tangu kuanza kazi baraza jipya la mawaziri la serikali ya Benjamin Netanyahu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu (Israel); ambapo katika kipindi hicho kumeshuhudiwa mivutano zaidi ya ndani na mapigano kati ya Wazayuni na Wapalestina.  

Katika upande wa ndani, wazayuni wamekuwa wakiandamana mara kwa mara dhidi ya Netanyahu na baraza lake la mawaziri huku makumi ya maelfu ya watu wakiandamana katika miji mbalimbali nyakati za usiku. 


342/