Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

6 Februari 2023

16:07:07
1344089

Waislamu wa Nigeria waadhimisha miaka 44 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran

Maadhimisho ya kuwadia miaka 44 ya ushindi ya Mapinduiz ya Kiislamu ya Iran yamefanyika kwa shangwe ya aina yake katika jimbo la Bauchi nchini Nigeria.

Maelfu ya Waislamu katika jimbo hilo wamehudhuria maadhimisho ya miaka 44 ya ushindi ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yaliyopata ushindi mwaka 1979 kwa uongozi wa Imamu Ruhullah Khomeini.

Akizungumza na Shirika la Habari la Iran Press, Sheikh Luqman Abdallah Abdallah, mwanazuoni wa Jimbo la Bauchi kuhusiana na taathira ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran nje ya mipaka ya Iran amesema, Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran yamekuwa na taathira na mwamko barani Afrika ikiwemo Nigeria.

Aidha mwanaharakati huyo wa Kiislamu amesema kuwa, kuanzishwa harakati za Kiislamu kama Harakati ya Kiislamu ya Nigeria inayoongozwa na Sheikh Ibrahim Zakzaky, ni moja ya matokeo na taathira za Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. 

Kwa upande wake Bi Khadija Adam, mmoja wa wanaharakati wa Kiislamu katika jimbo la Bauchi ameashiria umuhimu mkubwa ulionayo Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran na kueleza kwamba, kufanikiwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran maana yake ni kufanikiwa Waislamu wote ulimwenguni.

Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini Iran yaliyoongozwa na Imamu Ruhullah Khomeini, mwasisisi na mwanzilishi wa jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalihitimisha utawala wa kitaghuti wa Kipahlavi uliokuwa unaungwa mkono kila upande na madola ya kibeberu yakiongozwa na Marekani.

342/