Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

10 Februari 2023

20:39:31
1345305

Kosa la "AI chatbot" lalitia hasara ya dola bilioni 100 shirika la Google

Shirika kubwa la Google limepata hasara ya zaidi ya dola bilioni 100 katika thamani ya soko lake Jumatano baada ya chatbot yake ya bard kuonyesha taarifa za uongo.

Mashirika mbalimbali yameripoti habari hiyo likiwemo shirika la habari la Fars, shirika la habari la NPR la Marekani na shirika la habari la Reuters la nchini Uingereza na kuongeza kwamba, hitilafu za Alfabeti zilizotokea katika tangazo la Google siku ya Jumatatu limelitia hasara ya zaidi ya dola bilioni mia moja shirika hilo.

Mashirika hayo yameongeza kuwa, hisa katika kampuni mama ya Alfabeti ya Google zilishuka kwa asilimia 8, au $8.59, hadi $99.05 kwa kila hisa, baada ya kushindwa kujibu swali kuhusu ni satelaiti gani ilichukua picha ya kwanza ya sayari ya ziada ya jua. 

Hapo awali Google ilitoa video fupi ya GIF ya Bard kupitia Twitter, ikieleza kwamba chatbot ni ukurasa unaosaidia kupatika kiurahisi maudhui ngumu. Baada ya Microsoft kutangaza mipango yake ya kuunganisha "chatbot erevu" ya mshindani wake ChatGPT kwenye injini yake ya utafutaji ya Bing na bidhaa nyingine; shirika la Google lilihisi hatari na liliamua kuzindua chatbot ya Bard.

Katika tangazo la chatbot ya Bard ya Google, mtafutaji anaelekezwa kwenye swali linalosema: Ni uvumbuzi gani mpya kutoka kwa Darubini ya Anga ya James Webb (JWST) ninayoweza kumwambia mtoto wangu wa miaka 9? "Bard Chatbot" inajibu kwa vidokezo vichache, ikiwa ni pamoja na kudai kwamba "darubini hiyio ya JWST ndiyo iliyochukua picha za kwanza kabisa za "exoplanets," au sayari zilizoko nje ya mfumo wa jua wa dunia." Jibu hilo si sahihi, kwa sababu picha za kwanza za sayari za nje ya mfumo wa jua wa dunia zilichukuliwa na Darubini Kubwa Sana ya Uangalizi wa Kusini mwa Ulaya (VLT) mwaka 2004.

342/