Main Title

source : ABNA24
Jumamosi

11 Februari 2023

10:26:45
1345418

Wairani washiriki kwa wingi katika maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu

Sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini zimeanza mapema leo kote nchini kwa ajili ya kuadhimisha miaka 44 ya mapinduzi hayo hayo, huku miji na vijiji vyote vya Iran vikishuhudia maandamano makubwa kuelekea viwanja na maeneo ya umma.

Mamilioni ya Wairani wanashiriki katika sherehe hizo za tarehe 22 Bahman (Februari 11) ili kusisitiza mshikamano wao mkubwa, kizazi baada ya kizazi, na thamani za Mapinduzi ya Kiislamu, wakipeperusha bendera ya Uislamu na kuzidisha matumaini ya kupata ushindi watu wote wanaokandamizwa na kudhulumiwa duniani.

Sherehe za mwaka huu za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran zina ladha ya kipekee, hasa baada ya kufeli njama kubwa iliyoanzishwa na madola ya kigeni dhidi ya Iran ya Kiislamu katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, iliyolenga usalama wa ndani na umoja na mshikamano wa taifa kwa kuibua ghasia na kuziunga mkono kupitia vita mseto vya kisiasa, kiuchumi na hujuma ya vyombo vya habari vya Magharibi. Hata hivyo hujuma na vita hivyo vilishindwa kutokana na mwamko, umakini, kusimama kidete, umoja na mshikamano wa wananchi na hekima ya viongozi wao.

Ushiriki mkubwa wa mamilioni ya wananchi wa Iran katika maandamano na sherehe za leo za kuadhimisha ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu unatoa pigo kubwa zaidi kuliko miaka ya nyuma kwa mabeberu wa kimataifa, ambayo bado hawajafahamu hali halisi ya Iran ya Kiislamu tangu baada ya Mapinduzi hayo hadi hizi sasa.

Miongoni mwa programu za maadhimisho ya mwaka huu ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ni kuimba kwa pamoja wimbo wa taifa wa Iran kote nchini kulikofanyika saa 11:22 (kwa wakati wa Tehran).

Habari zaidi kuhusu maadhimisho ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini zitakujieni katika matangazo yetu yajayo.

342/