Main Title

source : Parstoday
Jumapili

12 Februari 2023

15:22:19
1345742

Visa vya kujitoa uhai vyakithiri kwa kiwango cha kutisha Marekani

Matokeo ya utafiti uliofanya huko Marekani yanaonyesha kuwa, idadi ya Wamarekani wanaojitoa uhai imeongezeka kwa kiwango cha kutisha, huku vijana wa Kimarekani wenye asili ya Afrika wakiongoza kwenye orodha hiyo.

Takwimu mpya zilizotolewa na Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini humo (CDC) zinaonesha kuwa, idadi ya Wamarekani waliojiua mwaka 2021 ni 48,183, ikilinganishwa na 45,979 mwaka 2020 na 47,511 mwaka 2019.

CDC inasema kuwa, aghalabu ya kesi za kujitoa uhai zilizoshuhudiwa mwaka 2021 ni miongoni mwa vijana weusi wa kiume, waliokuwa na umri kati ya miaka 10 na 24.

Kituo cha Kuzuia na Kudhibiti Magonjwa nchini Marekani kimesema kuwa, kujitoa uhai ndiyo sababu kuu ya pili ya vifo miongoni mwa vijana wenye miaka baina ya 10-34 nchini humo.

Julie Goldstein Grumet, Naibu Rais na Mkurugenzi wa taasisi ya Zero Suicide Institute katika Kituo cha Ustawi wa Elimu amesema kuwa, inavunja moyo kuona ongezeko hilo la kutisha la watu haswa vijana wanajiua ni wa jamii au kundi moja la Wamarekani.

Serikali ya Rais Joe Biden wa Marekani pia ilitangaza karibuni kwamba, mzozo wa afya ya akili katika jamii ya nchi hiyo umeongezeka kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa tena huko nyuma.

Ukubwa wa tatizo hilo unaonyesha kuwa jamii ya Marekani sio tu inakabiliwa na mgogoro wa afya ya akili, bali migogoro ya kijamii na kisiasa ambapo mabadiliko ya haraka ya kijamii pia yamekuwa na taathira kubwa zinazoathiri afya ya akili ya watu wa nchi hiyo na hasa tabaka la vijana.


342/