Main Title

source : Parstoday
Jumatano

22 Februari 2023

17:55:13
1348316

AU yawataka wanachama wake kukata uhusiano na Israel kutokana na 'ukoloni' wake huko Palestina

Umoja wa Afrika (AU) umeziomba nchi wanachama kukata uhusiano wa kisayansi na kitamaduni na utawala wa Kizayuni wa Israel hadi utawala huo utakapokomesha sera za "ukoloni" dhidi ya Palestina.

Mapendekezo hayo yamo katika tangazo lililowasilishwa kwa nchi wanachama mwishoni mwa mkutano wa hivi majuzi wa Umoja wa Afrika, ambapo wajumbe wa utawala wa Israeli walitimuliwa kutoka kwenye ukumbi mkutano baada ya kuingia bila idhini.

Katika kikao cha hivi karibuni Umoja wa Afrika haukuchua uamuzi kuhusu ombi la utawala haramu wa Israel kuwa mwanachama mwangalizi. Badala yake kilichoshuhudiwa ni nchi za Afrika kueleza misimamo imara dhidi ya Israel kutokana na vitendo vyake vya kinyama dhidi ya watu wa Palestina.

Tamko la AU limesema kikao cha wiki iliyopita "kimeziomba nchi wanachama kukomesha biashara zote za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja, mabadilishano ya kisayansi na kitamaduni na utawala wa Israel."

Ingawa baadhi ya nchi wanachama wa AU tayari zina uhusiano wa kisayansi na Israel ushauri wa kukata uhusiano huo ni pendekezo zito zaidi dhidi ya Israel tangu Umoja wa Afrika ulipoundwa miaka 21 iliyopita

Katika lugha kali isiyo ya kawaida, Umoja wa Afrika ulilaani kile ilichokiita "mienendo ya wakoloni wa Israel katika maeneo ya Palestina inayoyakalia kwa mabavu, kuwabagua Wapalestina kwa misingi ya rangi na dini, na kuwapa Waisraeli haki na upendeleo zaidi juu ya Wapalestina ambao ni wamiliki wa ardhi wa Palestina."

342/