Main Title

source : Parstoday
Jumatano

22 Februari 2023

17:59:24
1348323

Mshauri mkuu wa Rais wa Senegal anawasili Tehran leo akiongoza ujumbe wa ngazi za juu wa nchi yake

Kaimu wa Mkuu wa Klabu ya Biashara ya Iran na Afrika amesema kuwa, ujumbe wa ngazi ya juu wa kiuchumi wa Senegal ukiongozwa na mshauri mkuu wa rais na mkuu wa muungano wa wafanyabiashara wa nchi hiyo unawasili mjini Tehran leo kwa ajili ya kuimaimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa pande mbili.

Sayyid Ruhollah Latifi, Kaimu wa Mkuu ambaye pia ni msemaji wa Klabu ya Biashara ya Iran na Afrika, amelithibitishia taarifa hiyo, shirika la habari la Mehr na kusema: Ujumbe wa wafanyabiashara wa Senegal utakutana na mashirika ya biashara na uzalishaji ya Iran katika ziara ya kikazi itakayodumu kwa muda wa siku 10.

Mheshimiwa Sheikh Sisse, Mshauri Mkuu wa Rais wa Senegal katika masuala ya uchumi na ambaye pia ni mkuu wa chama cha wafanyakazi wa nchi hiyo, ndiye anayeongoza ujumbe huo wa kiuchumi na kibiashara wa Senegal katika ziara yao hapa nchini Iran.

Ameongeza kuwa: Ziara ya ujumbe huo wa Senegal imetokana na mwaliko wa Klabu ya Biashara ya Iran na Afrika na unajumuisha makampuni ya magari, vitengo vya uzalishaji wa chuma, makampuni ya uzalishaji wa chakula na mauzo ya nje, makampuni ya uzalishaji wa matunda na mboga mboga, vitengo vya uzalishaji wa vitambaa na nguo, vitengo vya uzalishaji wa mafuta ya petroli na bidhaa mbalimbali za viwandani. Ujumbe huo utatembelea maeneo ya uzalishaji wa mazulia, makampuni ambayo msingi wake ni elimu na maarifa, vitengo vya uzalishaji wa unga wa maziwa na kufanya mazungumzo na vitengo vya tasnia ya madini na mashirika ya kitaifa ya kilimo na chakula ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

342/