Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

27 Februari 2023

16:34:56
1349481

Zaidi ya watu elfu sita wameuawa kwa bunduki Marekani katika chini ya miezi miwili

Taasisi moja ya Marekani imetangaza kuwa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, zaidi ya watu elfu sita wameuawa kwa silaha za moto nchini humo.

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Uswisi linalohusika na masuala ya umiliki wa bunduki, linalojulikana kama "Small Arms Survey", Marekani ndiyo nchi pekee duniani ambako idadi ya silaha ni kubwa kuliko idadi ya watu; Kuna takriban bunduki 120 mkabala wa kila watu wazima 100 wa Marekani.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanywa na taasisi ya Marekani "Gun Violence Archive", tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2023 hadi sasa, yaani chini ya miezi miwili, zaidi ya watu elfu sita na mia sita wameuawa kwa silaha za moto kote Marekani, idadi ambayo ni wastani wa vifo 116 kwa siku.

Rripoti hiyo imesema, kuanzia Januari hadi Februari mwaka huu, kumekuwapo matukio 84 ya ufyatulianaji wa risasi nchini Marekani, ambayo taasisi ya Gun Violence Archive inasema ni sawa na mauaji ya watu wasiopungua wanne  kwa klila tukio moja."

Ulinganisho wa takwimu za mashambulizi ya bunduki kati ya Marekani na nchi nyingine duniani unaonyesha kuwa Marekani ni nchi ya kipekee kabisa katika uwanja huu. Kiwango cha mauaji ya silaha za moto katika nchi hiyo ni kikubwa zaidi kuliko nchi nyingine yoyote duniani na takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha sasa cha mauaji ya watu wa bunduki nchini Marekani ndicho cha juu zaidi ikilinganishwa na miaka 30 iliyopita. 

342/