Main Title

source : Parstoday
Jumatatu

27 Februari 2023

16:36:18
1349484

Waislamu watakiwa kususia tende za Israel mwezi wa Ramadhani

Kampeni mpya ya kususia utawala wa Kizayuni imezinduliwa ili kuwataka Waislamu barani Ulaya na maeneo mengine duniani kuangalia lebo za matunda hasa tende na kuepuka kununua tende za utawala haramu wa Israel katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waislamu wanapaswa kuhakikisha kuwa hawafuturu kwa bidhaa za "ubaguzi wa rangi," waandaaji wa kampeni hiyo wamesema.

"Kwa kuchagua kutonunua tende za Israel katika mwezi huu wa Ramadhani, Waislamu wanaweza kutuma ujumbe wa wazi na wenye nguvu wa kulaani vitendo vya Israel uvamizi na ukaliaji haramu, l na ubaguzi wa rangi huko Palestina," alisema Shamiul Joarder wa Jumuiya ya Marafiki wa Al-Aqsa (FOA) yenye makao yake nchini Uingereza.

Taarifa hiyo imebaini kuwa "Israel ndio mzalishaji mkubwa zaidi duniani wa tende aina ya Medjool, na asilimia 50 ya tende za Israeli zinauzwa Ulaya. "Tende hizi zinauzwa katika maduka makubwa makubwa pamoja na maduka madogo katika bara zima la Ulaya."

Jumuiya ya Marafiki wa Al-Aqsa imeongeza kuwa asilimia kubwa ya tende za Israel zinazosafirishwa kwenda Ulaya huuzwa Uingereza, Uholanzi, Ufaransa, Uhispania na Italia. Mnamo 2020 Uingereza iliagiza zaidi ya tani 3,000 za tende kutoka Israeli, zenye thamani ya takriban pauni milioni 7.5.

Taarifa hiyo pia imebainisha kuwa hadi sasa mwaka huu, Israel imewaua shahidi Wapalestina wasiopungua 62 wakiwemo watoto 13 - sawa na mtoto mmoja kila baada ya siku tano.

Siku ya kuwahimiza Waislamu "kuangalia lebo" (#CheckTheLabel ) imeandaliwa kwenye misikiti ya Uingereza mnamo Machi 17, Ijumaa ya mwisho kabla ya Ramadhani. Pia kutakuwa na harakati ya mtandaoni ya uhamasishaji wikendi ya mwisho kabla ya mwezi mtukufu wa Ramadhani.

342/