Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

3 Machi 2023

13:57:32
1350204

Rais wa Baraza la Usalama UN akwepa kujibu suali kuhusu Palestina na Ukraine

Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa amekataa kujibu suali aliloulizwa kuhusu Palestina na Ukraine.

Pedro Comissário Afonso, Rais wa zamu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na balozi wa kudumu wa Msumbiji katika Umoja wa Mataifa, amekwepa kutoa jibu la wazi kwa suali aliloulizwa na ripota wa gazeti la Al-Quds al-Arabi kuhusu muelekeo wa kiundumakuwili wa jamii ya kimataifa kuhusiana na Palestina ikilinganishwa na Ukraine.Akijibu suali la kushindwa Umoja wa Mataifa kutatua masuala yanayohusiana na Ukraine na Palestina, Pedro Commissario Alfonso amesema kushindwa huko hakujaathiri itibari ya Umoja wa Mataifa, 

Awali katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Palestina ililitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liheshimu ahadi na majukumu yake na kuchukua hatua za kutekeleza maazimio yake hususan azimio nambari 2334 kuhusu uharamu wa ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Wapalestina.

Tarehe 23 Disemba 2016, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia azimio namba 2334 liliutaka utawala haramu wa Kizayuni wa Israel usimamishe mara moja na kikamilifu shughuli zake zote za ujenzi wa vitongoji vya walowezi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.Utawala wa Kizayuni unaendelea kujenga vitongoji vya walowezi wa Kizayuni bila ya kujali matakwa ya jamii ya kimataifa na unaungwa mkono na Marekani katika suala hilo.../


342/