Main Title

source : Parstoday
Ijumaa

3 Machi 2023

13:58:01
1350205

Rais wa Mexico: Taifa langu lina demokrasia kushinda Marekani

Rais Andrés Manuel López Obrador wa Mexico amesema taifa lake lina demokrasia zaidi ya Marekani, katika kile kinachoonekana ni kuzidi kuingia doa uhusiano wa nchi mbili hizo.

Rais wa Mexico amesema hayo baada ya maafisa wa Marekani kutoa matamshi ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo ya Amerika ya Latini.

Amesema, "Kuna demokrasia ya kiwango cha juu nchini Mexico kushinda Marekani. Nina ushahidi wa kuthibiti kuwa kuna uhuru na demokrasia hapa Mexico zaidi ya Marekani."

Kauli ya Rais Mexico inakuja siku chache baada ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Ned Price kutoa matamshi ya kukosoa mageuzi ya hivi karibuni kwenye mfumo wa upigaji kura nchini Mexico.

Sehemu ya mageuzi hayo ni kuipinguzia bejeti Tume ya Uchaguzi ya Mexico. Rais López Obrador amekanusha madai ya maafisa wa Marekani kwamba mageuzi hayo yatalemaza demakrasia, na kusisitiza kuwa pesa zilizopunguzwa kwenye taasisi hiyo zitaelekezwa kuwanufaisha maskini.

Mara kwa mara wananchi wa Mexico wamekuwa wakifanya kampeni ya kususia bidhaa za Marekani na vile vile  maandamano ya kupinga sera za Washington, haswa za kuzuia wakimbizi wa Kimexico kuingia nchini Marekani. 


342/