Main Title

source : Parstoday
Jumamosi

4 Machi 2023

16:54:06
1350504

Uraibu wa vikwazo, Marekani yayawekea vikwazo makumi ya mashirika ya China, Pakistani na Russia

Ikiwa ni kuendelea na ugonjwa na uraibu wake wa vikwazo, Idara ya Biashara ya Marekani imeyawekea vikwazo makumi ya mashirikika ya China, Russia, Belarus na Pakistan na kuyaingiza kwenye orodha yake ya marufuku ya kibiashara.

Shirika la Habari la Fars News limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, Marekani imeendelea na uraibu wake wa vikwazo kwa kuyawekea vikwazo mashirika 37 ya nchi ambazo hazikubaliani na sera zake za kibeberu. Imeweka vikwazo hivyo kwa kisingizio cha eti kulinda maslahi yake ya kitaifa na kiusalama, 

duru za habari zimeripoti kutoka Washington DC kwamba, Idara ya Biashara ya Marekani imesasisha orodha yake ya pande zilizo marufuku kufanya nazo biashara na kuongeza mashirika 37 ya kigeni katika orodha hiyo.

Kwa upande wake, shirika la habari la Reuters limeripoti habari hiyo kwa kusema, mashirika 37 ya China, Russia, Belarus, Pakistan, Myanmar, Taiwan na nchi nyingine yameongezwa kwenye orodha hiyo ya Idara ya Biashara ya Amerika. 

Kati ya mashirika hayo, 28 ni ya China, manne ni ya Pakistan, matatu ni ya Myanmar, shirika moja moja kwa kila nchi za Russia na Belarus na moja la Taiwan.

Kampuni ya "BGI Group" ya China, na "DMT Electronics" ya Russia ni miongoni mwa makampuni ambayo yaliyomo kwenye orodha hiyo mpya ya vikwazo vya Marekani. 

Katika ripoti yake kuhusu hatua hii ya Washington, shirika la habari la Reuters limeweka pia majina ya idadi kubwa ya makampuni ya Kichina yaliyoimo kwenye orodha nyeusi ya Idara ya Biashara ya Marekani.Kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari vya Magharibi, hatua hii mpya ya Marekani bila ya shaka itaongeza mvutano kati ya Washington na Beijing; nchi mbili ambazo zinapamba katika vita vya teknolojia tena kwa miaka kadhaa sasa.

342/